Timu anayochezea aliyekuwa nyota ya Manchester United na baadae Real Madrid na Ac Milan ya Italy na aliepata kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza David Beckham, Los Angels Galaxy almaarufu kama LA Galxy imefankiwa tena kunyanyua kombe la ligi ya Marekani maarufu kama MLS Cup kwa mwaka wa pili mfufulizo na hata hivyo huu ndio utakuwa mwaka wa mwisho kwa nyota huyu kucihezea timu hiyo tokea alipojiunga nayo miaka sita iliypita.
Kwa kunyanyuua ubingwa huo timu ya LA Galaxy ilifanikiwa kuifunga timu ya Houston Dynamo mabao 3-1 katika fainali iliyochezwa jana usiku katika uwanja wa nyumbani wa LA Galaxy ujulikanao kama Home Depot Center kwa mabao mawili yaliyopatikana kwa njia ya mikwaju ya penati toka kwa nahodha wao Landon Donovan na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ireland na Totenham Hospurs ya Uingereza Robbie Keane.
 |
David Behakam akinyanyua juu kombe la MLS Cup juu mbele ya umati wa mashabiki wao, picha zote kwa hisani ya mtandao wa www.thesun.co.uk |
 |
Beckham akionyesha furaha kutokana na kunyakua kombe kwa mara ya pili mfufulizo |
 |
Beckham akiwapungia mashabiki wake katika kusherehekea ushindi wao |
 |
Beckhama akiwa katika moja ya hekaheka za uwanjani katika mchezo wao na Houston Dynamo |
 |
Beckham akizeeka na uhodari wake wa kupiga mipira iliyokufa maarufu kama Free Kicks |
No comments:
Post a Comment