MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Thursday, 22 August 2013

Maeneo ya Dar yakosa umeme baada ya moto kuunguza mitambo ya SonGas Ubungo.

Posted on 22:46 by Unknown
Mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas iliyopo Ubungo jijini dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo imeungua moto kabla ya kudhibitiwa na Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto kwa kushirikiana na kikosi cha Kampuni ya Knight Support.
Picture
Askari wa Kikosi cha zimamoto na Uokoaji wakizima moto uliokuwa unawaka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas, Ubungo jijini Dar es Salaam. (Picha: Francis Dande

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Felichesim Mramba, alisema hitilafu hiyo imetokea katika kituo cha 33kv na kusababisha gridi ya taifa inayotumika jijini Dar es Salaam kuzimika, hivyo baadhi ya maeneo umeme ukawa umekatika.

“Tulipata taarifa saa 10 kuwa kuna hitilafu hapa na tukajaribu kuwasiliana na Idara ya Zimamoto kwa simu wakawa hawapatikani mpaka tulipowafuata ofisini kwao. Nashukuru baada ya taarifa walifika kwa wakati na wakafanikiwa kuudhibiti moto,” alisema.

Alisema kuwa kutokana na hitilafu hiyo maeneo mbalimbali ya jiji yaliyokuwa yakipata umeme kupitia kituo
 hicho yataathirika na kuyataja kuwa ni Kigogo, Mburahati, Magomeni, Tandale na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Meneneo mengine ni Changanyikeni, Kimara, Tabata na Riverside na kwamba juhudi zinafanyika kuangalia uwezekano wa maeneo hayo kuunganishwa katika njia nyingine kwa muda.

Aliongeza kuwa bado hawajajua thamani halisi ya hasara iliyopatikana na muda utakaotumika kufanya marekebisho huku akiainisha kuwa ukarabati wa vifaa hivyo unaweza kuchukua wiki moja mpaka mbili kutegemea na aina ya uharibifu.

Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa moshi uliokuwa ukitoka katika mitambo hiyo ulikuwa mzito na uliwasababishia kushindwa kupumua vizuri.

“Niliwaona kina mama na watoto waliokuwa wanakwenda katika kituo cha mabasi Ubungo wakipata taabu kupumua hadi tukawa tunawasaidia kuwapeleka mbali na eneo la tukio,” alisema Gervas Lutabalize, ofisa wa Chama cha kutetea abiria.

Kamanda wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji jijini Dar e s Salaam, ACP Jesward Ikonko, alisema walipata taarifa ya tukio saa 11:58 alfajiri na kufika katika tukio saa 12:5 ambapo waliwakuta wafanyakazi wa kikosi cha Knight Support wakiwa wameshaanza kazi ya kuzima moto. --- via Habari Mseto blog

Source: http://www.wavuti.com

































































Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Habari | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Administration Officer
    Administration Officer Moshi Urban Water Supply and Sewerage Authority (MUWSA) Date Listed: Sep 5, 2013 Email...
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • RAFA BENITEZ Akalia kuti kavu
    RAFA Benitez kocha wa muda wa Chelsea jana amekiri ya kwamba siku zake zimeshaanza kuhesabika ndani ya timu hiyo kutokana na matokeo mabaya ...
  • Michezo ya Ligi kuu ya Uingereza wikiendi hii katika Picha
    Everton 2 Liverpool 2 Luis Suarez akishangilia goli kwa mtindo wa kuruka mbele ya kocha wa  Everton David Moyes ikiwa kama majibu kulingana ...
  • Website Designer
    Website Designer House of Graphics Date Listed: Mar 8, 2013 Email Address: Click to Email Phone: P...
  • Monetary Boards in collaboration to support development and growth.
    Leaders of the African Development Bank, European Bank for Reconstruction and Development, Inter-American Development Bank, International Mo...
  • VIDEO: Obama dancing along to Tanzania’s brass dancers
  • Weighbridge Operator - (Eight Posts)
    Weighbridge Operator - (Eight Posts) Tanzania National Roads Agency (TANROADS) Date Listed: Sep 4, 2013 Phone...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ▼  August (18)
      • USAJILI WA GARETH BALE KWENDA REAL MADRID WAIVA
      • Chelsea join race for Willian,Bale's Madrid move i...
      • Maeneo ya Dar yakosa umeme baada ya moto kuunguza ...
      • Benki ya Taifa Biashara yazindua kampeni ya kuweka...
      • Real Madrid are rumoured to be holding the number ...
      • Just like OBAMA and OPRAH , Robert Kelly will aslo...
      • Oprah tells her Serengeti trip story through photos
      • Wenger kumgeukia Michu
      • MIWANI PANA YA EDO ~ TATHMINI YA MECHI YA KWANZA Y...
      • University of Dar es Salaam among top 100 Universi...
      • Cristiano Ronaldo's future at Real Madrid remains ...
      • THIAGO ALCANTARA KULETA MZOZO BAYERN!!
      • Clinton atua Dar kiaina
      • Vichwa vya Magazeti leo kuhusu usajili Barani Ulaya
      • REAL MADRID NA MANCHESTER UNITED KWENYE MAZUNGUMZO...
      • Real Madrid stars worried Ronaldo will leave
      • Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani
      • Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile