MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Thursday, 5 September 2013

Wabunge wa Upinzani nchini Kenya wasusia kikao cha Bunge

Posted on 08:01 by Unknown
Baadhi ya wabunge wa upinzani nchini Kenya wameondoka bungeni wakati mjadala mkali ukiendelea kuhusu kuunga mkono au kupinga nchi hiyo kujiondoa kutoka katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
 
Ukumbi wa Bunge la Kenya
Wabunge hao wameondoka bungeni baada ya kusema kuwa kamwe hawataungana na upande wa serikali kuunga mkono hoja hii ya kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC.Ni kutokana na kuwa kwamba upinzani una idadi ndogo zaidi ya wabunge bungeni.
Naibu kiranja wa wabunge walio wachache bungeni Jakoyo Midiwo, alisema kuwa wabunge wa upande wa serikali wanaotetea hoja hii ya kujondoa Hague watakuja kujuta. Mjadala huu unatokana na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kukabiliwa na kesi za uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama hiyo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008Hatua hii ya wabunge inakuja zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa Kenya Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Rais Uhuru Kenyatta pia anatarajiwa kufika katika mahakama hiyo mwezi Novemba kwa kesi dhidi yake.Wawili hao wanashtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2007.Msemaji wa ICC ameambia BBC kuwa kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Bwana Fadi El Abdallah, alisema kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote ile kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri tu kesi zilizokuwa mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.

Hii ni hatua ya dharura inayochukua serikali kujitoa katika Mkataba wa Roma wa mahakama hiyo ulioidhinishwa na Umoja wa mataifa mnamo tarehe 17 July, mwaka1998.

Kenya inataka kutoa mfano wa kuwa nchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hiyo licha ya kwamba uamuzi huu hautoathiri kwa namna yoyote kesi zinazoendelea sasa katika mahakama ya ICC.

Mahakama hiyo ya kimataifa imesema kwamba kesi hizo zitaendelea hata iwapo Kenya itajitoa.Imesema itaichukua Kenya kiasi ya mwaka mmoja kabla ya kukubaliwa ombi hilo la kutaka kujiondoa katika mkataba wa Roma na hilo litaathiri tu kesi zitakazozuka baada ya muda huo.

Haya yanajiri wakati makamu wa rais William Ruto anatarajiwa kuondoka Kenya kueleka Hague Uholanzi wiki ijayo kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadaamu katika mahakama hiyo ya ICC, kesi inayoanza tarehe 10 mwezi huu.

Wote wameshtakiwa kwa kuhusika katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.Kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Novemba.

Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in East Africa News | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ▼  September (9)
      • ABIDAL: BARCELONA HAWAKUNILIPA HATA SENTI TANO MIE...
      • Kikwete, Kagame come face to face in Kampala
      • Weighbridge Operator - (Eight Posts)
      • Administration Officer
      • Sales & Marketing Officer 1 (Four Posts)
      • Wabunge wa Upinzani nchini Kenya wasusia kikao cha...
      • Nani kaingia na nani katoka_Usajili vilabu vya Uin...
      • Tempetation
      • JINSI MABOSI WANAVYOTUMIA VYEO KULAZIMISHA NGONO
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile