Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
Kanisa lililojengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya makanisa ya kale yaliyojengwa enzi za ukoloni yapata miaka 100 ambapo watemi wa kabila la wasukuma walikuwa wakiabudu .
Ni kama kigoda vile umbo la jengo hili ambako ndiko kulitumika kuhifadhi ngoma za asili zilizotumiwa na wanasanaa wa kabila la Wasukuma katika koo mbalimbali ngoma hizi zimehifadhiwa yapata miaka 100 sasa . Mdau Madata Ndelule Charles mhifadhi mwandamizi wa makumbusho hayo akionyesha mfano wa nyumba ambayo watemi waliishi.
Bagika na Bagalu ni ngoma za pande mbili ndani ya kabila la Wasukuma ambapo Bagika walikuwa wakicheza ngoma inayoshirikisha nyoka na Bagalu walikuwa wakicheza ngoma inayoshirikisha zana kama majembe ya mkono, zana za kale za kivita.Kikundi cha sanaa cha Bujora group
Zana na nyenzo za enzi za kale zilizotumika katika usagaji nafaka ili kupatikana unga.
Hatua kwa hatua usagaji nafaka kwa kutumia zana na kale huku nyimbo asili zikitawala .Habari na picha kwa msaada wa blogu ya http://netnewstz.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment