MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Friday, 24 May 2013

Mtwara: Askari watuhumiwa kubaka, kumwua mjamzito, kupora, kuchoma nyumba moto .

Posted on 01:29 by Unknown



Picture
Askari wakiwa lindoni/doriani, Mtwara

Hali ya usalama katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani hapa imezidi kuwa mbaya baada ya askari polisi kudaiwa kufanya unyama kwa kuwabaka wanawake na kumpiga risasi mjamzito

Mbali na unyama huo polisi pia wanadaiwa kuchoma moto nyumba tatu za wananchi katika mtaa wa Magomeni na vibanda vya maduka kadhaa na kupora vitu vilivyomo ndani.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa anasema hali ni shwari na kwamba wananchi watoke nje kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Picture 
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi amethibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, zinazoaminika kuwa za risasi na hivyo kufanya idadi ya maiti zilizopokelewa hospitalini hapo kufikia mbili na majeruhi 18: “Ni kweli kwa leo tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa miezi saba, amepigwa risasi tumboni...” “...pia tumepokea mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Chuno, amevunjwa miguu yote kwa risasi.”

Habari zinadai kuwa mjamzito huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake baada ya polisi kuvamia makazi yake.

Huduma za kijamii zimesimama, hakuna maduka yaliyo wazi, hakuna usafiri wa daladala wala pikipiki, mji upo kimya, sauti za milio ya mabomu na bunduki zimetawala, wanajeshi waliovalia sare wameuzingira mji wakiwa katika magari na pikipiki.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti wakazi hao wamelalamikia kitendo cha askari wa jeshi la polisi kuingia katika makazi yao, kuwapiga, kuwabaka na kuwapora mali zao:


“Magomeni A hatuna amani askari wanaingia majumbani mwetu wanatupiga na kutunyang’anya simu, yani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepoteza watoto na hatujui hata waume zetu wako wapi” alisema Paulina Idd na kuongeza: “Majumba yetu yamechomwa moto wanaofanya fujo ni polisi wenyewe halafu wanakuja wanatubaka na kuiba mali zetu halafu tunateseka sisi yaani tumechoka kabisa na serikali yenyewe,” alisema Paulina.



Kamanda Sinzumwa alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa atapingana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Mchimbi aliyewasili Mtwara leo: “Kuhusiana na suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa kwani nitapingana na Waziri wangu kwani leo ametoa tamko bungeni na leo atawasili,” alieleza Sinzumwa

Wakazi wakimbia maeneo yao
Wakazi wa maeneo mbalimbali wamekimbia makazi yao hususani wanawake na watoto na kuhamia hospitali ya rufaa kwa kuhofia usalama wao huku wengi wao wakipotezana na ndugu zao.

Hali hiyo imetokea kufuatia kuwepo kwa milipuko ya mobomu katika maeneo mbalimbali mjini hapa huku huduma za kijamii zikiwa bado zimesitishwa. Hali hiyo imetokea baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vilivyokuwa vikihamasisha wananchi wa mkoani hapa kusitisha huduma zote hapo jana  ili kusikiliza hotuba ya wizara ya nishati na madini.

Kufuatia hali hiyo imesababisha kifo kwa raia mmoja aliyefahamika kwa jina Karim Shaibu (22) mkazi wa Chikongola ambaye alipigwa risasi wakati wa fujo kati ya jeshi la polisi na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mganga mkuu wa mkoa hospitali ya rufaa ya Ligula Dk Sadun Kabuma alithibitisha kupokea kwa kifo hicho ikiwa ni pamoja na majeruhi 17 wakiwemo askari watatu: “Ni kweli jana kuanzia majira ya saa 10 hadi saa 11 nilipokea majeruhi 17 ambapo kati ya hao wamishtuko ni wanawake watano na askari watatu na kijana mwingine ambaye alikuwa na jeraha na katika harakati zan kumwokoa maisha yake alifariki akiwa chumba cha upasuaji,” alisema Dk Kabuma

Wananchi wazungumzia bajeti

Wakizungumzia uwasilishwaji wa hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini wakazi wa hapa wamesema kuwa hawakubaliani na ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwani mpango huo utawaletea dhuluma: “Mpango wa kusafirishwa kwa gesi asilia hatuna mpango nao kwa wakazi wote wa Mtwara kwa kifupi akina mama wa mtwara hatutaki itoke,” alisema Fatuma Abdallah.


.........................

Imenukuliwa kutoka mtandao wa www.wavuti.com









































































































Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Habari | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ▼  May (91)
      • Real Madrid yapatwa na kigugumizi
      • Parallel institutions vital to monitor tax adminis...
      • Agents told to exploit opportunities in insurance ...
      • Sida dishes out USD 10m to support agricultural gr...
      • Medical in Charge Emergency Medical Department Muh...
      • Office Administrator
      • Mourinho arudi zake Chelsea, Bale kuuzwa kwa paund...
      • Robin van Persie shows amazing skills v kids....
      • The Government has been urged to protect local in...
      • Dar es Salaam Goat Races to take part on 1st June ...
      • Jeshi lafanikiwa kudhibiti vurugu Mtwara
      • Neymar amua kuelekea Barcelona
      • Bayern Munich Mabingwa wapya wa Ulaya, Neymar aele...
      • Adnan Januzaj - Manchester United 2013
      • Dar Looks Forward to Obama's Tour
      • African Must Improve Livestock Data
      • Safari lager beer wins top Africa awards
      • Polisi kawe wabambikizia watu kesi
      • The implementation of 400 MW gas-fired power proje...
      • Kenyan celebrities at MTV All stars’ red carpert
      • HARUNA NIYONZIMA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC
      • Bingwa wa Europa kuingia mojamoja Champions Ligi k...
      • Mtwara: Askari watuhumiwa kubaka, kumwua mjamzito,...
      • Kocha wa Malaga, Manuel Pellegrini kubwaga manyang...
      • Maonyesha ya 8 ya Vyuo Vikuu ya TCU yaanza rasmi j...
      • Picha za Mpambano baina ya Yanga na Simba
      • Torres kufungashiwa virago vyake dirisha la usajili
      • Zantel rewards winners of ‘Recharge and Win’ promo...
      • This week Sports on The Rumor Mill
      • Kandoro apongeza ushindi Safari Lager
      • Alex Ferguson's final Press conference
      • OMBI KWA MHE RAIS JAKAYA KIKWETE OKOA ARDHI YETU N...
      • BSL Interpreter / Tanzanian Orphanage
      • Linah, Barnaba kutimuliwa THT
      • Weigh Bridge Operators (3 Posts)
      • Administrative Assistant
      • David Beckhma hatiamye atundika daluga rasmi....
      • Sales Officers with AKIBA Commercial Bank PLC.
      • Bank Tellers Vacancy Posts
      • Community Relations Manager – (One Post)
      • Bookings and Marketing Officer
      • Vodacom na Samsung zazindua S4 nchini Tanzania
      • Angelina Jolie akatwa matiti kuzuia Saratani
      • Beckham aweka Rekodi mpya
      • Man Utd lift Premier League trophy
      • Ngono zembe ilivyokithiri barabara ya kuelekea Zambia
      • Roberto Mancini atolewa nishai na Roberto mwenzake
      • Mariah Carey - #Beautiful ft. Miguel
      • David Moyes, kocha mpya wa Mabingwa wa Uingereza a...
      • Finance Manager-ActionAid Tanzania
      • Operation Supervisors-Tanzania International Conta...
      • Monitoring and Evaluation Officer
      • Financial Controller
      • Human Resources and Administration Officer
      • Tanzania has a long bilateral relations with Arabs
      • Goat charity races to raise billions for community...
      • Youth jobs’ gains wiped out by slow recovery
      • AJIRA KWA VIJANA ZAATHIRIWA NA UKUAJI MDOGO WA UC...
      • Donors pledged Tsh 800bn in the general budget sup...
      • Sir Alex Fergsuon Angatuka MAnchester United
      • Accounts Officer
      • Accountant(s)-Vacancy
      • Human Resources and Administration Officer
      • ILO report shows why social protection is crucial ...
      • The East African Round Up
      • Afdb organizes pan-African training workshop
      • Competitive private sector a key to economic growth
      • African financial markets launch its website
      • Vodacom, GNLD signs deal to help clients
      • Nini Chanzo cha Tamaa ya Ngono
      • KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA...
      • Huyu Ndiye Gareth Bale...
      • Mbatia ataka Kawambwa si tu ajiuzulu, bali ikiweze...
      • Workers around the globe divine on decent jobs.
      • CCM top echelons connected to illegal ivory dealing.
      • TPC set aside incentives to motivate its workers
      • TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU (...
      • Mourinho awataka Frank Lampard na John Terry kubak...
      • Assistant F&B Manager
      • Consultant for End Term Evaluation (Tandahimba Com...
      • Accountant
      • Administration Secretary
      • Website Administrator/Customer Care
      • Marketing and Sales personnel.
      • Information Technology Manager
      • Serikali yachukua uamuzi mgumu, yafuta matokeo
      • Real Madrid wamtaka Chicharito kwa Paundi ml 25
      • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho y...
      • Rapa wa Kriss Kross afariki Dunia jijini Atlanta
      • Discover new ideas, technologies and business oppo...
      • UFALME wA SOKA LA UHISAPNIA WAKARIBIA UKINGONI.
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile