MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Saturday, 4 May 2013

TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU (THRD-COALITION) KUPINGA KUKAMATWA KWA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WILAYA YA BAHI

Posted on 01:55 by Unknown

Tanzania Human Rights Defenders Coalition [THRD-Coalition]
P. O. Box 105926 Dar es Salaam, TANZANIATelephone: +255-22-2773038/48, Fax: +255-22-2773037, Mob: +255 783 172394 E-mail:  defenderscoalition@rocketmail.com, web  www.thrdcoalition.com 


TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU (THRD-COALITION) KUPINGA KUKAMATWA KWA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WILAYA YA BAHI 
BB DOMINIC HAULE NA WENZAKE SITA

Mtandao wetu umezipokea kwa majonzi habari za kukamatwa kwa mwanachama wake na Mtetezi wa Haki za Binadamu BB Dominic Haule na wenzake sita. Waliokamatwa ni Mpumba Mwaruko, Juma Kamunya, Charles Munyakongo, Ayubu Mukosi, Matereka Ndoru, na Champunga Mburi Mutinya.

Taarifa tulizozipokea kutoka eneo hilo zinasema Bw Haule na wenzake wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa kutimiza majukumu yao kama raia wema wanaotaka kuona kwamba utawala wa sheria na haki unazingatiwa. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu hivyo vya habari watetezi hao wakiwamo waandishi wa habari walikuwa wanafuatilia mambo yaliyokuwa yanalalamikiwa na wananchi ambayo ni pamoja na kutozwa michango mikubwa bila kuona manufaa ya kile wanachochangia.

Baadhi ya maeneo yaliyokuwa yanaathiriwa na ukiukwaji huo wa haki za binadamu ni Kijiji cha Chali Isanga, Wilayani Bahi ambalo ni eneo lililo chini ya uangalizi wa Utetezi wa Haki za Binadamu wa Bw BB Dominic Haule. Vyanzo vyetu vinaeleza kwamba ukiukwaji huo ni pamoja na watu kutozwa hadi shilingi la saba kwa mtu mmoja kwa ajili ya michango hiyo kulingana na idadi ya mifugo aliyonayo.


Pia kulikuwa na fedha zilizokuwa zimechangwa kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule pamoja na Wadi ya Kujifungulia akina mama kijijini hapo bila kukamilika. Katika ujenzi huo jengo hiloliliezekwa kwa mabati ya zamani na kupakwa rangi huku ikielezwa kuwa ni mapya jambo ambalo wananchi walilipinga.

Pia katika hatua hiyo ilibainika kwamba baadhi ya vifaa vya ujenzi vimeuzwa na baadhi ya viongozi wa kijiji kwa watu wasiohusika na katika kutaka kufukia habari hiyo wakaamua kuzuia waandishi wasijue chochote

Mnamo tarehe 24 Aprili Bw BB Dominic alitafuta mwandishi wa habari na kwenda naye kijijini na wakati wakiwa kijijini hapo katika kazi ya uchunguzi walikutana na wananchi waliowapa ushirikiano na kuwaonyesha baadhi ya vifaa vya ujenzi wa zahanati vilivyoibwa na viongozi na kuuzwa kwa watu wasiohusika.



--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Board of Directors:
Dr. Helen Kijo Bisimba, Kharous Mpatani, Martina Kabisama, Tike Mwaipabipile, Joseph Parsambei,
Saed Kubenea, Hamisa Mmanga and Ernest Kimaya.


Wakati wakihojiana na wanavijiji hao, alifika Afisa Mtendaji wa Kata (WEO), na kuanza kuhoji uhalali wa mwandishi wa habari kufika kijijini hapo ambapo alimtaka aonyeshe kitambulisho chake cha kazi.

Huku akiwa ni mwenye hasira kali na kwa woga wa kuumbuliwa katika vyombo vya habari alikitupa chini kitambulisho hicho na akakipiga teke kisha kumpiga ngumi mwandishi huo wa REDIO KIFIMBO na kusababisha kupoteza baadhi ya vifaa vyake vya kazi.

Kitendo cha kupigwa kwa mwanahabari Maliki Selemani kiliwakera wananchi na hasa baada ya kuona kwamba waliyemtegemea kulinda amani ndiye anakiuka haki za binadamu na kumpiga mwandishi asiye na hatia. Na hapo ikatokea purukushani kati ya wanakijiji na mtendaji huyo. Baada ya tukio hilomtendaji huyo wa Kata ya Chali Isanga alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na siku ya pili yake alifika akiwa na askari na kuanza kuwakamata baadhi ya wananchi.

Inadaiwa kukamatwa huko kunafuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa, hadi sasa Mtetezi BB Dominic na wananchi wengine sita wamekamatwa, kufunguliwa shitaka la uchochezi na kusababisha vurugu kijijini. Baada ya kukamatwa walipelekwa Dodoma mjini kwa uchunguzi zaidi kutokana na tukio hilo.

Baada ya kufanyika jitihada wakiwa katika kituo cha Bahi na kwa kuhofia kwamba kitendo cha kuendelea kumkamata mwandishi wa habari kingeleta kelele nyingi mwandishi huyo aliachiwa na kubakizwa Mtetezi wa Haki za Binadamu BB Dominic na wananchi hao sita. Mpaka sasa wahusika bado wako kizuizini na hawana msaada wowote na kwa taarifa tulizonazo wamebambikiziwa kesi nyingine ya kujeruhi.

RAI YETU

•       Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu haujaridhishwa na mazingira ya kukamatwa kwa mwanachama wake na wananchi waliotajwa kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, kila mwananchi anahaki ya kupata taarifa sahihi za mapato na matumizi ya serikali katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na vijiji halmashauri za wilaya na serikali kuu. Lengo likiwa ni kuzingatia uwazi ambayo ni nguzo muhimu katika kulinda utawala bora.

•       Tunalitaka Jeshi la polisi Mkoani Dodoma na Wilayani Bahi watimize majukumu yaokisheria na kuacha kutumika na baadhi ya viongozi was serikali wasiojua misingi ya utawala bora na haki za binadamu.

•       Mtandao wa Watetezi unalitaka Jeshi la Polisi kuwaachia huru watetezi hao kwani makosa waliyotuhumiwa kwa malengo ya kuwaridhisha watawala katika eneo la Bahi yanaruhusu dhamana.

•       Tunawataka viongozi wote wa serikali wenye nia mbaya dhidi ya watetezi wa haki za binadamu hapa nchini kuacha mara moja kutumia vyombo vya dola kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu. .

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Board of Directors:
Dr. Helen Kijo Bisimba, Kharous Mpatani, Martina Kabisama, Tike Mwaipabipile, Joseph Parsambei,
Saed Kubenea, Hamisa Mmanga and Ernest Kimaya.


•       Pia Mtandao unawasihi viongozi wote waheshimu kazi za waandishi wa habari kwani kitendo cha Afisa Mtendaji wa Kata kumpiga ngumi mwandishi wa habari na kukanyaga kitambulisho chake ni kunyume na utawala bora na kuingilia uhuru wa habari.






Onesmo Olengurumwa



MRATIBU MTANDAO WA
WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU.









































--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Board of Directors:
Dr. Helen Kijo Bisimba, Kharous Mpatani, Martina Kabisama, Tike Mwaipabipile, Joseph Parsambei,
Saed Kubenea, Hamisa Mmanga and Ernest Kimaya.






















































Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Announcement | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ▼  May (91)
      • Real Madrid yapatwa na kigugumizi
      • Parallel institutions vital to monitor tax adminis...
      • Agents told to exploit opportunities in insurance ...
      • Sida dishes out USD 10m to support agricultural gr...
      • Medical in Charge Emergency Medical Department Muh...
      • Office Administrator
      • Mourinho arudi zake Chelsea, Bale kuuzwa kwa paund...
      • Robin van Persie shows amazing skills v kids....
      • The Government has been urged to protect local in...
      • Dar es Salaam Goat Races to take part on 1st June ...
      • Jeshi lafanikiwa kudhibiti vurugu Mtwara
      • Neymar amua kuelekea Barcelona
      • Bayern Munich Mabingwa wapya wa Ulaya, Neymar aele...
      • Adnan Januzaj - Manchester United 2013
      • Dar Looks Forward to Obama's Tour
      • African Must Improve Livestock Data
      • Safari lager beer wins top Africa awards
      • Polisi kawe wabambikizia watu kesi
      • The implementation of 400 MW gas-fired power proje...
      • Kenyan celebrities at MTV All stars’ red carpert
      • HARUNA NIYONZIMA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC
      • Bingwa wa Europa kuingia mojamoja Champions Ligi k...
      • Mtwara: Askari watuhumiwa kubaka, kumwua mjamzito,...
      • Kocha wa Malaga, Manuel Pellegrini kubwaga manyang...
      • Maonyesha ya 8 ya Vyuo Vikuu ya TCU yaanza rasmi j...
      • Picha za Mpambano baina ya Yanga na Simba
      • Torres kufungashiwa virago vyake dirisha la usajili
      • Zantel rewards winners of ‘Recharge and Win’ promo...
      • This week Sports on The Rumor Mill
      • Kandoro apongeza ushindi Safari Lager
      • Alex Ferguson's final Press conference
      • OMBI KWA MHE RAIS JAKAYA KIKWETE OKOA ARDHI YETU N...
      • BSL Interpreter / Tanzanian Orphanage
      • Linah, Barnaba kutimuliwa THT
      • Weigh Bridge Operators (3 Posts)
      • Administrative Assistant
      • David Beckhma hatiamye atundika daluga rasmi....
      • Sales Officers with AKIBA Commercial Bank PLC.
      • Bank Tellers Vacancy Posts
      • Community Relations Manager – (One Post)
      • Bookings and Marketing Officer
      • Vodacom na Samsung zazindua S4 nchini Tanzania
      • Angelina Jolie akatwa matiti kuzuia Saratani
      • Beckham aweka Rekodi mpya
      • Man Utd lift Premier League trophy
      • Ngono zembe ilivyokithiri barabara ya kuelekea Zambia
      • Roberto Mancini atolewa nishai na Roberto mwenzake
      • Mariah Carey - #Beautiful ft. Miguel
      • David Moyes, kocha mpya wa Mabingwa wa Uingereza a...
      • Finance Manager-ActionAid Tanzania
      • Operation Supervisors-Tanzania International Conta...
      • Monitoring and Evaluation Officer
      • Financial Controller
      • Human Resources and Administration Officer
      • Tanzania has a long bilateral relations with Arabs
      • Goat charity races to raise billions for community...
      • Youth jobs’ gains wiped out by slow recovery
      • AJIRA KWA VIJANA ZAATHIRIWA NA UKUAJI MDOGO WA UC...
      • Donors pledged Tsh 800bn in the general budget sup...
      • Sir Alex Fergsuon Angatuka MAnchester United
      • Accounts Officer
      • Accountant(s)-Vacancy
      • Human Resources and Administration Officer
      • ILO report shows why social protection is crucial ...
      • The East African Round Up
      • Afdb organizes pan-African training workshop
      • Competitive private sector a key to economic growth
      • African financial markets launch its website
      • Vodacom, GNLD signs deal to help clients
      • Nini Chanzo cha Tamaa ya Ngono
      • KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA...
      • Huyu Ndiye Gareth Bale...
      • Mbatia ataka Kawambwa si tu ajiuzulu, bali ikiweze...
      • Workers around the globe divine on decent jobs.
      • CCM top echelons connected to illegal ivory dealing.
      • TPC set aside incentives to motivate its workers
      • TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU (...
      • Mourinho awataka Frank Lampard na John Terry kubak...
      • Assistant F&B Manager
      • Consultant for End Term Evaluation (Tandahimba Com...
      • Accountant
      • Administration Secretary
      • Website Administrator/Customer Care
      • Marketing and Sales personnel.
      • Information Technology Manager
      • Serikali yachukua uamuzi mgumu, yafuta matokeo
      • Real Madrid wamtaka Chicharito kwa Paundi ml 25
      • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho y...
      • Rapa wa Kriss Kross afariki Dunia jijini Atlanta
      • Discover new ideas, technologies and business oppo...
      • UFALME wA SOKA LA UHISAPNIA WAKARIBIA UKINGONI.
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile