MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Friday, 11 January 2013

Makampuni ya Oman yatangaza kuwekeza ATCL bilioni 160

Posted on 05:44 by Unknown
MUUNGANO wa makampuni kadhaa kutoka nchini Oman, umetangaza uwekezaji wa kihistoria kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Muungano huo, umekusudia kutoa Sh bilioni 160 kwa ajili ya mambo mbalimbali, yakiwamo ya kununua ndege mpya na za kisasa na ujenzi wa kituo cha mafunzo.

Hatua hiyo, imekuja baada ya ziara iliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete, nchini Oman Oktoba mwaka jana, ambapo alitoa fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta za maendeleo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Hayat Development, Sheikh Salim Al Harthy, alisema hatua ya uwekezaji huo, utasaidia kufungua milango kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.

Alisema makubaliano hayo, yamefikiwa na Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said Sultan wa Oman. Alisema katika sehemu ya kwanza ya kujitolea kwa nchi hiyo, itaingia makubaliano ya kusaini mkataba maalum kuisaidia ATCL, kwa kuwekeza Dola za Marekani milioni 100 na kuongeza ndege za makampuni mengine. Alisema uwekezaji huo, utakwenda sambamba na ununuzi wa ndege ambazo zitatumika katika safari za ndani na nje ya Afrika.

“Kutokana na ziara ya Rais Jakaya Kikwete katika nchi ya Oman, Oktoba mwaka jana, alifanikiwa kufanya mazungumzo kwa kirefu na Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said Sultan, na kukubaliana uamuzi wa kuwekeza nchini.

“Kabla ya makubaliano haya, yalifanyika makongamano mengi nchini Oman, ambayo yalishirikisha makampuni mbalimbali, sasa yameamua kuutumia muungano wao na kufanya uwekezaji mkubwa kwa nchi yetu.

“Uwekezaji huu mkubwa kwa ATCL, utafungua njia za kibiashara kwa kuwa na ndege za kisasa, ambazo zitafanya biashara ya kubeba abiria ndani ya nje ya nchi.

“Tunamshukuru Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said wa Oman na Rais Kikwete, kutupatia nafasi hii, hasa ukizingatia kipindi hiki tuna mpango wa kujenga kituo cha mafunzo ya masuala ya ndege kwa ATCL.

“Mbali na hili, tutajenga ofisi ya kisasa ambayo itakuwa kwa ajili ya matumuzi ya shirika hili la ndege ya Tanzania, pamoja na kufanya shughuli nyingine za maendeleo tunazotarajia kuanza ndani ya miezi sita hadi kumi kutoka sasa,” alisema.

Sheikh Salim Al Harthy, alisema uwekezaji huo, ni matokeo mazuri ya mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Serikali ya Oman.

Mwaka jana, Rais Kikwete alipotembelea Oman, baada ya kualikwa na Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said, ambapo aliambatana na ujumbe wa mawaziri na viongozi waandamizi wa biashara. Katika ziara hiyo, Rais Kikwete alibadilishana uzoefu wa uhusiano na kuangalia namna ya kudumisha ushirikiano wa nchi hizo, kuhusiana na biashara, elimu na utamaduni. Ziara ya Rais Kikwete katika nchi ya Oman ni ya pili kufanyika, baada ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kutembelea nchi hiyo, mwaka 1985.

Source: by wavuti
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Local News | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ▼  January (14)
      • The government has assured women entrepreneurs
      • Tanzania Emerged in top Ten for Ibrahim Index Afri...
      • Dirisha Dogo la Usajili lafungwa Rasmi....Pata Kuj...
      • Sauti za Busara kuanza Valentine Day
      • “Doing Business and Measuring Business Regulations...
      • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
      • Post: Part-time journalist
      • Mario azua fujo mjini Milan
      • Vikao vya Mtwara: Viongozi wa Dini, Jamii watoa do...
      • Balotelli says Goodbye
      • MSAMAHA
      • Makampuni ya Oman yatangaza kuwekeza ATCL bilioni 160
      • Oil & Gas, HSE Supervisor, Tanzania
      • I Am In Love by The Ben
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile