MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Wednesday, 30 January 2013

Sauti za Busara kuanza Valentine Day

Posted on 22:52 by Unknown
Sauti za Busara yaanza kwa Busara Xtra
Tamasha la muziki la Sauti za Busara linatarajiwa kuanza  tarehe 14 ya mwezi wa pili na kuufanya mji mkongwe wa Zanzibar kung’ara kwa mara nyingine tena. 

Ni siku ya kwanza ya ‘Busara Xtra’, siku ambayo Mji Mkongwe utasheheni maonesho ya biashara mbalimbali za sanaa na burudani, ngoma, na madarasa ya kucheza muziki, sambamba na muziki wa reggae ambao utatumbuiza huku ukipata mandhari nzuri ya kuzama kwa jua. Siku hii yenye mvuto wa kipekee ya maonesho ya sanaa itafanyika  katika mgahawa wa Livingstone ambapo itaanza tarehe 14 Februari na kuendelea kwa siku zote za tamasha, sambamba na kuwepo kwa vinywaji vya aina mbalimbali, ambapo shughuli zote hizi zitaanza saa 4 asubuhi.



Itawawia vigumu kwa wahudhuriaji kuchagua ni wapi pa kwenda, kwani kutakuwa na burudani kabambe katika maeneo mbalimbali, wakati muziki wa Reggae utaanza saa 10 za jioni huko Kae Funk Michamvi, Nadi Ikhwan Safaa kikundi maarafu cha muziki wa Taarabu hapa Zanzibar kitafanya onesho lake NIS Club House, onesho litakaloanza saa 10 za jioni. Bado kutakuwa na kazi ya ziada kuchagua kwenda kwenye muziki wa Taarabu wa zamani wa asili au kwenda katika onesho la Sinachuki Kidumbak Taarabu ya kisasa, ambapo burudani zote hizi zitakuwa Mji Mkongwe,  ndio maana Busara Xtra ipo kwa ajili yako. 

Nae Mkurugenzi wa tamasha la muziki la Sauti za Busara Yusuf Mahmoud amesema kwamba, tamasha mara zote limekuwa likilenga katika kuwanufaisha wazanzibar, tokea tamasha lianze mwaka 2004 idadi ya wageni wanaoitembelea Zanzibar mwezi wa pili imeongezeka hadi kufikia asilimia tano, pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali na ajira kwa wazanzibar na kuongezeka kwa wageni kila mwaka, kwa kiasi kikubwa Sauti za Busara imekuwa ikisaidia watu wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla. Kuwepo kwa Busara Xtra pia inachangia kukuza uchumi na utamaduni wa kisiwa cha Zanzibar. “Busara Xtra inaongeza fursa kwa wasanii wageni kuonesha kazi zao, wageni kutembelea maeneo mbalimbali ya kisiwa cha Zanzibar, kukutana na wazanzibari na kuongeza ushikiri katika tamasha kwa jamii ya wazanzibari wa kawaida.

Baada ya kujumuika na tamasha la Busara Xtra, jukwaa kuu la Sauti za Busara litafunguliwa tarehe 15 ya mwezi wa pili na kuendelea na burudani mpaka tarehe 17 mwezi wa pili 2013. Pia ratiba ya filamu ya Busara imepangwa kuonyesha filamu tatu ambazo zitakamilisha jukwaa la muziki. Kwa upande wa amphitheatre hapo Ngome Kongwe kutaoneshwa filamu za wasanii mbalimbali maarufu wa muziki, pamoja na filamu ndefu. Kwa maelezo zaidi au kununua tiketi mtandaoni, tafadhali tembelea wovuti ya www.busaramusic.org au nunua tiketi mlangoni kuanzia tarehe 13 mwezi wa pili 2013. Tiketi ni shilingi 3000 kwa watanzania na kiwango maalumu kwa wanaotoka Afrika Mashariki.

Sauti za Busara inawashukuru  kipekee wadhamini wote ambao ni  Goethe Institute, Grand Malt, Memories of Zanzibar, Diamond Trust Bank, ChemiCotex, Azam Marine, Ultimate Security, Zanzibar Unique Ltd., Southern Sun, Embassy of France, Alliance Française, SMOLE II na wengine wote kwa kufanikisha tamasha la mwaka huu. 


Kwa maelezo zaidi na picha downloads:  Tafadhali tembelea wovuti ya www.busaramusic.org
* Picha za Hi-resolution kwa waandishi wa habari zinnaweza kupatikana kwa maombi.
Tunaendelea na kuboresha na kuorodhesha orodha ya annuani zetu za barua pepe tulizonazo
this list is only to be used for providing information to press people
Jarida hili la barua pepe limetumwa kwa dmakangale1@yahoo.com. Unauwezo wa kujiengua kutoka katika listi yetu la jarida hili, kwa kutembelea (URL) kisara hiki: http://www.busaramusic.org/cgi-bin/dada/mail.cgi/u/habari/
Kama kisara (url) hiki hakibofyeki, chukua muda kunakili kisara hiki kizima kwani wasomaji wengine wa barua pepe hii wanaweza kuuvunja mstari huu kua mistari kadhaa

Unaweza kuwasiliana nasi kwa anuani pepe hii press@busara.or.tzNa kwa wale wanaoweza kutumbelea tupo, njia ya kuelekea uwanja wa ndege tukiangaliana upande wa pili wa barabara na Gofu club Maisara
Busara Promotions, mkabala na Golf Club, Maisara, Njia ya uwanja wa ndege, Zanzibar, Tanzania

Mailing List Powered by Dada Mail

Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Burudani | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ▼  January (14)
      • The government has assured women entrepreneurs
      • Tanzania Emerged in top Ten for Ibrahim Index Afri...
      • Dirisha Dogo la Usajili lafungwa Rasmi....Pata Kuj...
      • Sauti za Busara kuanza Valentine Day
      • “Doing Business and Measuring Business Regulations...
      • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
      • Post: Part-time journalist
      • Mario azua fujo mjini Milan
      • Vikao vya Mtwara: Viongozi wa Dini, Jamii watoa do...
      • Balotelli says Goodbye
      • MSAMAHA
      • Makampuni ya Oman yatangaza kuwekeza ATCL bilioni 160
      • Oil & Gas, HSE Supervisor, Tanzania
      • I Am In Love by The Ben
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile