MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Saturday, 9 March 2013

Tamko Kuhusu kuvamiwa na kupigwa kwa Mr. A. Kibanda

Posted on 04:06 by Unknown


TAMKO LA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUFUATIA SHAMBULIO LA KIKATILI DHIDI YA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI BW. ABSALOM KIBANDA
Machi 07, 2013

Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ambao ni kusanyiko la zaidi ya asasi 70 za kiraia  zinazotetea haki za binadamu  chini ya mwamvuli wa THRD-Coalition unalaani vikali shambulio la kinyama alilofanyiwa mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda usiku wa kuamkia jana Jumatano tarehe 6 Machi, 2013.  

Usiku wa kuamkia tarehe 6/3/2013 Bwana Kibanda alivamiwa wakati alipokuwa anarudi nyumbani kwake Mbezi juu. Watu hao walimteka na kisha wakamtesa kinyama kwa kumng’oa meno, kucha,  kidole na kuliharibu vibaya sana jicho la upande wa kushoto. Huu ni ukatili, unyuma dhidi ya utu wa binadamu.Baada ya kutekeleza azma yao walimtupa umbali wa mita 30 toka alipokuwa amepaki gari lake. 

Uchunguzi tulioufanya bado haujatujapatia habari za undani zaidi na za uhakika wa tukio hilo. Lakini kwa taarifa za awali kwa asilimia kubwa  linahusiana na kazi yake ya utetezi wa haki za binadamu kupitia katika taaluma yake ya uandishi wa habari. Hii ni kwa sababu pia tayari alishafunguliwa kesi mahakani inayohusu uandishi wake.

Tunasema hivyo kwa sababu vitisho dhidi ya wanahabari na watetetezi wengine wa haki za binadamu vinataka kuzoeleka sasa hapa nchini jambo ambalo halikuwapo katika miaka ya nyuma. Takribani ndani ya miezi 10 sasa zaidi ya watetezi wa haki za binadamu  10 wakiwamo waandishi wa habari  wameshajeruliwa,  wamepata vitisho  na kuuwawa.

Matukio haya yanashiria  lengo la kutaka kuzima sauti za watetezi wa wanyonge kwa visingizio mbali mbali huku matukio ya aina hii wakati mwingine yakipewa sura tofauti tofauti ikiwamo uhalifu wa kawaida, visa vya kudhulumiana na  visasi vya kimapenzi. Ni dhahiri wanaofanya hivyo wana malengo mabaya ya kuchafua jina na taswira nzuri ya nchi yetu  katika Jamii ya Kimataifa kwa malengo binafsi.

Wakati tukio hili linapojitokeza sasa, bado Mtandao wetu unafuatilia kwa karibu kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi na mazingira ya kukamatwa na kuhojiwa kwa waandishi wa gazeti la Tanzania Daima kulikofanywa na Jeshi la Polisi hivi karibuni kwa kile kilichoitwa kwamba ni kuandika habari za uchochezi. 

Hatupendi kuingilia wala kukwamisha utendaji kazi wa jeshi hilo, lakini pia hatupendi wanahabari na watetezi wengine wafanye kazi yao katika mazingira ya woga. Tunaamini kwamba zipo njia muafaka zaidi za kushughulikia masuala yanayohusu taaluma ya habari. Kwa mfano lipo Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambalo linajukumu ya kusuluhisha migogoro inayohusiana na taaluma hiyo na iwapo itashindikana basi mhusika au wahusika bado wanakuwa na nafasi ya kwenda mahakamani. 

Kinachoshangaza ni kuona kwamba Jeshi la Polisi limefikia mahali pa kwenda kuwakamata waandishi na wahariri wa Tanzania Daima ndani ya chumba chao habari na kuwakagua hadi katika makazi yao na kuchukua nyaraka kadhaa kama ilivyotokea kwaa Bw. Josephat Isango.
Hali hiyo ya mahojiano ya kushtukiza na kuogofya imefanyika pia kwa wahariri Charles Misango na Edson Kamukara wote wa gazeti hilo, ambapo hatima yao bado haifahamiki mpaka sasa. Hali hii inaweza kusababisha woga kwa wanataaluma wengine na hivyo kuleta athari kubwa katika sekta ya habari nchini. 

Hata hivyo waandishi hao kwa sasa wanaishi kwa woga na kubadilisha vyombo vya usafiri pamoja na makazi ya kulala. Je kwanini tufikie hatua hii ya kufanya wenzetu waishi  kwa hofu kama suala kwenye mbuga iliiyojaa simba.Je ulinzi wa vyombo vya usalama upo kwa ajili ya nani? Kwanini wengine wauawe, watekwe, wateswe na kudhalilishwa  huku vyombo vya usalama vikichukulia ni jambo la kawaida na kutupiana mpira? 

Je nini Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla wamelifanya kuhusiana na kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka zaidi ya Kulifungia Mwanahalisi ambalo lilijitoa mhanga kuchunguza suala hili? Ndugu Kibanda katekwa na kufanyiwa kile kile alichofanyiwa Ulimboka, Je tume iliyoundwa  itaanzia kwa Ulimboka ama itarukia moja kwa moja tukio hili ambalo ni muoendelezo wa matukio lukuki dhidi ya watetezi wa haki na waandishi kwa ujumla.

Rai Yetu
1.     Tunawataka watu wote  wanaotumika au wanaoendeleza wimbi la mashambulizi kwa wanahabari na watetezi wote wa haki za binadamu kwa ujumla, waache kufanya hivyo kwani wataliingiza nchi katika machafuko makubwa. 

2.    Tunalisihi Jeshi la Polisi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kubeba jukumu lao la kuhakikisha usalama wa watetezi wa haki za binadamu, na raia na watu wote waliomo ndani ya mipaka ya nchi hii kwa ujumla bila ubaguzi.

3.    Tunaomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini wahusika wa mtindo huu wa kuteka kutesa na kutelekeza kwani tukio hili la Kibanda linashabihiana kwa kiwango kikubwa na lile la Dkt Stephen Ulimboka. 

4.    Tunaiomba jamii yote ya watu waliostaarabika, makundi mbalimbali kutuunga mkono katika jitihada zetu la kupigania amani, haki na uhuru kwa watu wote hasa hasa watetezi wa haki za binadamu na waandishi  wa habari.

5.    Tunawakumbushia waandishi wa habari kujitahidi kupata mafunzo ya usalama ambayo yanaratibiwa na kutolewa na Mtandao huu wa watetezi.

6.    Vyombo vyote vya habari  na  waandishi kwa ujumla wazidi kuwa pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kuelekea chaguzi za serikali za mitaa mwakani pamoja na uchaguzi mkuu 2015. Pia wajieupushe na makundi ya kisiasa ili kujiweka vizuri katika kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya taaluma zao.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!

Imeletwa kwenu na


Onesmo Olengurumwa
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa
Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition)
K.n.y Watetezi Wote wa Haki za Binadamu Tanzania
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Local News | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ▼  March (41)
      • Development Advisor (Governance and Cross Cutting ...
      • Graduate Trainees Oppurtunity
      • Accountants--Vacancy
      • Brazil vs Italy 2-2 All Goals FULL Highlights
      • Mario Balotelli - Crazy Boy
      • Ministers ordered to resign before taking up new jobs
      • Business leaders discuss recipes for job-rich grow...
      • Barclays Bank Tanzania Limited plans to increase i...
      • The East African Round Up
      • Branch Accountant (5 Post)
      • Customs Clearing & Forwarding Services
      • Website Designer
      • Volunteer, Malaria Case Management Analyst
      • Acountant Job Vacancy
      • Mvua yazidi kunyesha Dar
      • ERASMUS for ALL (2014-2020
      • Maonyesho ya Kusoma vyuo vya nje yamalizika rasmi
      • Street kids love sport!, Mwanza, Tanzania - CTBI C...
      • Secondary School Teaching in Tanzania, Tanzania - ...
      • Rio Ferdinand aitwa tena kuichezea timu ya Taifa y...
      • NEW Partnership for Africa’s Development Agency (N...
      • The East African Business Week
      • The East African Round Up
      • My Trip from Kigali, RWANDA
      • Papa Mpya huyu Hapa
      • Wakenya Walivyosherehekea ushindi wa Kenyatta
      • CORD kupinga matokeo ya urais makahamani
      • Uhuru Kenyatta Rais mpya wa Kenya
      • Tamko Kuhusu kuvamiwa na kupigwa kwa Mr. A. Kibanda
      • NIKE Kumrudisha RONALDO Man United kwa ada ya Paun...
      • Hesabu za kura 'zampa ushindi Kenyatta'
      • Fergie: Rooney will not be sold
      • Hali yazidi kuwa tete
      • UN agencies aims to generate new jobs and skills, ...
      • Uhuru Kenyatta mbele kwa hesabu
      • Rais wa Venezuela Hugo Chavez afariki
      • Anunua kwa Tsh milioni 2.5 mali ya Serikali yenye ...
      • Africa Tours Consultant
      • Mvua yazua Hali tete Jijini Dar es Salaam.
      • Country Directors (x6) (in Ethiopia, Malawi, Pakis...
      • Tanzania & Zanzibar Tailor-made Specialist - DCV T...
    • ►  February (59)
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile