MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Wednesday, 3 July 2013

Tofauti KUBWA kati ya Marekani na Tanzania.

Posted on 07:55 by Unknown
Ndugu zangu, 

Katika saa 20 na zaidi Rais Obama alipokuwa katika ardhi ya Tanzania, sikusikia mahali popote akitamka jina la chama chake cha Democrat. Obama ametamka ' AMERICA!' mara zisizohesabika.
Picture
Kwa kweli ujio wa Obama umetusaidia Watanzania kupumzika na kelele za vyama, maana, kwa siku kadhaa, kabla na wakati wa ujio wa Obama, Watanzania tumepata kupumzika na kusikia habari za vyama vya siasa na malumbano yasio na hoja za msingi, mara nyingi yasio na tija kwa nchi na maendeleo yake.

Hakika, siasa ni kitu kizuri sana kwa nchi. Lakini siasa za ' ovyo ovyo' ni kitu kibaya kwa nchi. Na mara nyingi, 
siasa za ' ovyo ovyo' ni kitu cha hatari kwa nchi na mustakabali wake.

Picha hiyo hapo juu ina mengi ya kutufundisha; kuwa siasa si uhasama. Uchaguzi ukiisha watu mnarudi kwenye kufanya kazi. Kupigania maslahi ya taifa. Si kuendeleza migogoro ya kisiasa na hata kuwepo kwa vurugu. Hayo hayana tija kwa nchi.

Unapomwangalia Obama na Bush kwenye picha ya pamoja wakiwa Dar na kwenye kutoa heshima kwa wahanga wa ugaidi kwenye mlipuko ulitokea kwenye Ubalozi wao mwaka 1998, inadhihirisha ukomavu wa kisiasa. 

Unachotumainia hapa, kuwa ifike siku, hata hapa kwetu Tanzania, kwa Rais aliye madarakani na Rais Mstaafu kutoka vyama viwili tofauti, tuone picha yao wakiwa wamesimama pamoja kwenye makaburi ya kumbukumbu ya mashujaa wetu wa Vita Vya Kagera kule Uganda.

Ndio, picha hiyo hapo juu ni somo kwetu. Hawa wawili; Bush na Obama, ndio tuliowaona kwenye kampeni zao wakipambana kiasi huwezi kufikiri wanaweza kusimama pamoja kama ndugu wa taifa moja.

Lakini, kwa wenzetu Marekani, siasa si uhasama wala mambo ya kuwindana. Wanachogombania kwenye siasa ni kupewa heshima ya kuitumikia Marekani. 

Na heshima hiyo akipata mpinzani wako, basi, kwa wenzetu wanachofanya ni kuungana mkono kwenye kazi ya maslahi ya Marekani bila kujali tofauti zao za kiitikadi. Na ndicho tunachofundishwa kwenye picha hiyo.

Swali linabaki, Watanzania tuko tayari kubadilika kifikra kwa maslahi ya taifa letu?
Picture
 
Maggid,
Iringa.
0754 678 252
mjengwablog.com

Source: www.mjengwablog.com
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Makala | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ▼  July (23)
      • Orodha ya TBS ya bidhaa 48 zisizotakiwa kuonekana ...
      • Madawa ya Kulevya Tanzania!
      • Kitchee FC vs. Manchester United 2:5 All Goals & H...
      • Fast-changing nature of world trade poses new poli...
      • Entrepreneurship skills vital in primary schools s...
      • EADB Receives EUR25 Million for SME Financing
      • MANCHESTER YAZIDI KUFANYA VIBAYA BAADA YAICHAPWA 3...
      • The East African Round Up
      • Mission Logistics Officer/ Receptionist
      • African Barrick Gold continues to support communit...
      • Smile for Tanzania education
      • SCHOLARSHIPS FOR TANZANIAN WOMEN
      • Chadema yaitesa CCM uchaguzi wa udiwani Arusha
      • Waliokamatwa na `unga`wa mabilioni ni mabinti
      • Neymar scores 45 yard goal in Lionel Messi charity...
      • Tofauti KUBWA kati ya Marekani na Tanzania.
      • Mabilionea Tanzania wakutana na Obama
      • 2013 Linux Foundation Linux Training Scholarship P...
      • ICT and Pedagogical Development 2013 C
      • Violent Episodes Grow in Tanzania, an African Haven
      • VIDEO: Obama dancing along to Tanzania’s brass dan...
      • Obama in Tanzania, sees Africa as next global econ...
      • Obama in Tanzania, sees Africa as next global econ...
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile