MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Thursday, 18 April 2013

Kitaifa Makinda kuamua hatima ya Lissu leo

Posted on 23:01 by Unknown
Chanzo cha kutimuliwa ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba (CCM).
 

Dodoma. Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema leo atatoa mwongozo kuhusu tukio la Naibu Spika, Job Ndugai kuwasimamisha wabunge sita wa Chadema.
Juzi, Ndugai aliwasimamisha wabunge hao Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiah Wenje (Nyamagana) na Godbless Lema wa Arusha Mjini kutohudhuria Bunge kwa siku tano kutokana na alichokiita kufanya vurugu ndani ya bunge.
Hatua hiyo ya Spika Makinda imekuja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kumtaka aeleze Ndugai alitumia kanuni gani kuwasimamisha wabunge hao.

Jana, baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbowe alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya 68(7) inayosema; “Hali kadhalika, Mbunge anaweza kusimama wakati wowote ambapo hakuna mbunge mwingine anayasema na kuomba “Mwongozo wa Spika” kuhusu jambo ambalo limetokea bungeni mapema, ili Spika atoe ufafanuzi kama jambo hilo linaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na majibu ya Spika yatatolewa papohapo au baadaye, kadri anavyoona inafaa.”
Mbowe alisema Kanuni ya 73(3) ndiyo inayompa ruhusa Naibu Spika na Spika kuwasimamisha wabunge na aliisoma: “Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda alipopewa amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.
“Kwa mujibu wa yaliyotokea jana (juzi) ilitokea sintofahamu katika matumizi ya kifungu hiki wakati tulitegemea Kifungu cha 74(1) ndicho kingetumika kwani kama mbunge amedharau mamlaka ya Spika jina lake linaweza kupelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,” alisema Mbowe na kuongeza: “Mheshimiwa Spika nataka mwongozo wako kujua Naibu Spika alitumia kanuni gani?”
Awali, Spika Makinda aliahidi kutoa mwongozo wake baadaye jioni kabla ya kuahidi kufanya hivyo leo wakati akiahirisha shughuli za Bunge jana.
Awali, baada ya mwongozo wa Mbowe, Spika Makinda alimruhusu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuomba mwongozo wake na aliposimama alisema: “Mwongozo wangu uko palepale katika kanuni ileile iliyoombwa na kiongozi wa kambi ya upinzani.”
Kabla hajamaliza, Spika alimkatisha na kumweleza kuwa hawezi kutoa nafasi ya mwongozo wa kitu hichohicho.
Alimruhusu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema ambaye alisema: “Waandishi walioandika kanuni hizi kwamba jambo lilitokea mapema hawakumaanisha jana.”
Kabla Jaji Werema hajamaliza, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisimama lakini Spika alimzuia na kuwakatisha wote akisema: “Waheshimiwa wabunge, hakuna kitu kinachowaharibia wananchi kama kilichotokea jana (juzi), jana (juzi) hakuna kitu kilichojadiliwa zaidi ya kuleta zahama.”
Nchemba tena
Alimruhusu Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba kuendelea kutoa mchango wake ambao ulikatishwa kutokana na vurugu za juzi na jana nusura tena tafrani izuke kati yake na Mnyika hasa baada ya Nchemba kueleza suala la mabaraza ya Katiba kuwa utaratibu ulipitishwa bungeni na wabunge wote.
Alisema kinachotaka kujengwa na wapinzani hakipo kwa kuwa katika Jimbo la Karatu lililoko chini ya upinzani, wenyeviti wa mabaraza ya Katiba walichaguliwa wa CCM.

chanzo: Gazeti la Mwananchi
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Local News | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ▼  April (53)
      • Charlie Chaplin - The Lion's Cage
      • Top 10: Wonderkids
      • Aston Villa yamdidimiza Paulo Di Canio 6-1 katika ...
      • Kenya & Tanzania Luxury Travel Specialist
      • Sales & Marketing Assistant
      • Volunteers
      • TPA Directors Vacancies
      • Alichozungumza kocha wa Arsenal, Arsene Wenger dhi...
      • Watanzania nchini China katika Sherehe za 49 Muungano
      • The East African Round Up -Waiganjo's case adjourned
      • Beyonce Knowles arudi rasmi jukwaan na awaacha hoi...
      • Kenya launches Gospel talent search
      • Kauli za Nyerere, Karume - 26.04.1964; Ndege za vi...
      • IMPORTANT REMINDER FOR STUDENTS AND ALUMNI: Comple...
      • AfDB launches project bonds in African markets
      • Mkutano wa CHADEMA Iringa, Jumanne 23.04.2013
      • African Barrick Gold (ABG) achieved strong perform...
      • Sir Alex Ferguson aongoza shamrashamra za ushindi
      • Man Utd win the Premier League - Custis verdict
      • Manchester United Mabingwa wapya wa Premier League...
      • Nafasi za Kazi
      • MWENYEKITI WA UMOJA WA SACCOS TAIFA MBEYA APIGWA...
      • Kumbe Luis Suarez akuanza jana kungata wenzake...A...
      • Luis Suarez bites Branislav Ivanovic
      • Manchester united kutangazwa Mabingwa endapo...
      • Administrative Assistant
      • Administrative Assistant, Family Medicine Entity
      • Manager Corporate Finance & Accounts
      • Programme Specialist - 'Electoral Support, Parliam...
      • Investment disputes brought to international arbit...
      • The East African Round Up
      • Kitaifa Makinda kuamua hatima ya Lissu leo
      • Marketing and Sales Executive
      • Administrative Officer (1 Post)
      • Data Entry Clerks (20 Positions)
      • Data Collectors (52 Positions)
      • Video: Dk Slaa (CHADEMA) atoa kauli nzito
      • Mbowe, Slaa: Hatukubali Chadema kuhujumiwa
      • Admission of Diploma holders into Higher
      • Scholarships for students and academics
      • Academic Research Proposal Writing For Postgraduat...
      • Vibwanga wvya mastaa wakisafiri
      • Governments have the primary responsibility for as...
      • DoubleTree by HIlton has partnered with Sober House
      • Head of Procurement Management Unit (One Post)
      • Kombe kuelekea Ujerumani au Uhispania..
      • Matthew Lowton Screamer goal Vs Stoke!!!!!
      • National Geographic Americas Hardest Prisons-State...
      • The BRICS group put forward the proposal establish...
      • BRANCH MANAGER
      • Job Advert
      • Maznat Bridal 10 Years Anniversary
      • Maznat Bridal 10 Years Anniversary
    • ►  March (41)
    • ►  February (59)
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile