MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Friday, 15 February 2013

Taarifa ya Katibu wa Bunge.

Posted on 07:25 by Unknown

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI

            Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyume na jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibu wa Bunge.

            Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge wala Kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katika Uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge.

            Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.

            Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwa kuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanza kurusha live video striping kupitia tovutiya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitia majadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti.

            Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bunge katika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kuna Radio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD, BBC, STAR etc.

            Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa na uwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwa moja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada ya mitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa.  Hivyo basi utaratibu uliopo sasa utaendelea kutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazo kwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazo yatakayotolewa na mitandao ya Bunge.

            Utaratibu huu unatokana na uamzi wa pamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bunge vitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwa juu ya mawasiliano TCRA.

            Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahiri kwua Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio au Tecknohama, bali  linatarajia kuboresha upatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pande zote, yaani Bunge na Wananchi.

            Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa, Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayo kwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake.  TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupata feedtoka katika mitambo ya Bunge, na pale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursa hiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya kambi la Bunge kwa minajiri hiyo.

            Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibu huo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani ya Kumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashi wao, watapata clear feed toka katika mitambo ya Bunge na hivyo kurusha live vipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa  kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali.  Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camera katika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasiliano itakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati.

            Hivyo basi, ili kwenda sawia na taratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habari za Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari, Idara ya Habari na Bunge lenyewe.

            Aidha ili kulinda heshima na maadili ya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Code of Conducts for Media broadcasting)wa namna ya kunakili na kurusha matangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi.  Hili litasaidia kuweka misingi bora ya mawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yote ndani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan).

            Hivyo basi, wakati zoezi la maboresho hayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwamba tunaendelea  kusisitiza tena, Wananchi wasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitisha matangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima la maboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge.

            Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibu wote walioakisiwa na taarifa hiyo.


Dr. Thomas D. Kashililah
KATIBU WA BUNGE

Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Habari | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ▼  February (59)
      • Fergie: Let me move upstairs
      • NBC APPOINTS NEW MANAGING DIRECTOR
      • Tanzania Portland Cement launches new expansion fo...
      • Kenya boy, 13, gains fame for protecting livestock...
      • Do not fight over land, says National Lands Commis...
      • Monetary Boards in collaboration to support develo...
      • Rais Kikwete akagua Ukumbi wa Kisasa wa Mikutano w...
      • ‘Kitanda kimoja wanalazwa watoto 4, mliyoikuta leo...
      • Heart suggery in Tanzania coming Soon...
      • Je huu ndio mwisho wa Ufalme wa Barcelona???
      • Accounts Receivables Manager
      • 2. Chief Operational Officer
      • Youth Civic Engagement Assistant Project Coordinat...
      • Customer Services / Marketing Administrator ? Clot...
      • Kesi dhidi ya Sh. Ponda: Serikali yafunga ushahidi.
      • Gareth Bale Goals 2012/2013
      • Are Spurs a one-man team?
      • Mancini zaidi ya Benitez, Swansea yafanya mauji ko...
      • Beckaham zaidi ya Joe Barton Ufaransa
      • Rafael amazing goal vs QPR 2013 & Man united vs Qpr
      • Ajali mbaya ya mashindano ya Magari yajeruhi watu 33
      • Mil 142/= zapatikana Mama Salma akiongoza hafla ku...
      • Yanga Yaididimiza Azam, Manchester yaendelea kupaa!!!
      • Accountant for Charity
      • Volunteer Accountant for Charity
      • Vibwanga vya Masta wa majuu katika picha
      • Africa Specialist Tailormade Travel Consultant - C...
      • Barcelona Chaliiiii mbele ya Ac Milan
      • The growth rate of world manufacturing output rema...
      • A major progress has been made on the fight agains...
      • Vibwanga vya Mastaa wa Majuu
      • Wanafunzi wajiua kwa kufeli mtihani wa Kidato cha ...
      • SASA MKAZO NI KUMALIZA NAFASI YA 4 BPL!!
      • SASA MKAZO NI KUMALIZA NAFASI YA 4 BPL!!
      • Supermario Balotelli
      • Taarifa ya Katibu wa Bunge.
      • Post: Part-time journalist
      • Oscar Pistorius arrested over fatal shooting
      • Huyu ndiye Mrembo aliyeuawa na Bingwa wa Olympic y...
      • Museveni abuses uniform -Besigye
      • 2 *PhD* Positions in Programming Language-based Se...
      • Job Advert--BBC Worldwide Limited.
      • Analyst/Economist Vacancy
      • Tahadhari kuhusu kupandishwa vyeo kupitia ujumbe w...
      • Digitali yavunja ndoa za watu uswahilini
      • Pope Benedict will Resigns on February 28th, 2013
      • Michezo mbalimbali ya mwishoni mwa wiki! katika Pi...
      • Nigeria Mabingwa wapya wa Africa 2013
      • Baada ya Jamie Caragger kutundika Daluga...wajue w...
      • Master in Leading Innovation and Change from York ...
      • Vibwanga vya mastaaa wa majuu
      • Mwanafunzi wa miaka 9 mbaroni kwa kumwibia mwallim...
      • Drogba 's reaction after papis cisses goal
      • Heavy Equipment Engineers
      • Tanzania 1 Cameroon 0
      • FNB Celebrated one Year in Tanzania
      • TPA and Mombasa Porty Authorithy on mission to cur...
      • Mario Balotelli anza kungaa Italia
      • Maandalizi ya Super Bowl Sunday Yapamba moto
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile