MAKANGALESOPHIE

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Wednesday, 20 February 2013

Wanafunzi wajiua kwa kufeli mtihani wa Kidato cha Nne.

Posted on 20:30 by Unknown
Matokeo mabovu --pengine-- kuliko yote ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne kuwahi kutokea katika historia ya taifa la Tanzania yamezua balaa la aina yake baada ya wanafunzi wawili kujiua kwa kujipiga vitanzi hadi kufa.

Taarifa zilizothibitishwa leo na jeshi la Polisi zimeeleza kuwa wanafunzi waliojiua kutokana na matokeo hayo ni wa jijini Dar es Salaam na mwingine kutoka mkoa wa Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,  Anthony Rutta, amesema leo kuwa mhitimu aliyejiua mkoani humo ni  Michael Fidelis (19) mkazi wa Mtaa wa Mwinyi, Kata ya Chemichemi aliyemaliza katika Shule ya Sekondari ya Kanyenye mjini Tabora.

Kamanda Rutta amesema kuwa Fidelis amejiua kwa kujinyonga hadi kufa baada ya kwenda kuangalia matokeo juzi Jumatatu (Februari 18, 2012), saa 11:00  jioni. Baadaye akakutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila, kisa ikiwa ni kupada divisheni ziro.

Taarifa kutoka kwa rafiki wa kijana huyo ambaye maziko yake yalifanyika juzi, zilisema awali alipigiwa simu na kaka yake aishiye Mbeya kumwambia kwamba matokeo yametoka.

Walisema wakiwa kwenye intaneti, kijana huyo ambaye ni wa kwanza kuzaliwa kwa mamake, alionekana amenyong’onyea, “Aliporudi nyumbani alinyong’onyea zaidi. Hakusema chochote. Kumbe alipotoka hapo alikwenda kujinyonga,” alisema mmoja wa watu waliokuwa naye.

Sehemu ya ujumbe alioacha marehemu Fidelis ulisomeka hivi: “Nisamehe sana mama, usitafute mchawi... nakupenda sana. Uamuzi niliouchukua ni sababu ya matokeo mabaya, nakutakia maisha mema.”

Matokeo ya shule ya Kanyenye yanaonyesha kuwa wahitimu 85 walipata sifuri na hakuna aliyefaulu kwa daraja la kwanza wala la pili.

Kwa mujibu wa ndugu zake, kijana huyo alikuwa akiishi na ndugu zake nyumba tofauti na mama yake ambaye alishaachana na baba yake mzazi na kuolewa na mume mwingine.  Ilielezwa kuwa alikuwa na kawaida ya kula usiku nyumbani kwa mama yake. Lakini usiku huo hakuonekana na ilipofika saa 3 usiku walikwenda na kukuta amejifungia ndani wakavunja mlango na kukuta amekufa.

Jijini Dar es Salaam, aliyejiua kwa kujipiga kitanzi baada ya kufeli ni aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Debrabant iliyopo Mbagala, wilayani Temeke, Barnabas Venant (18).

Kamanda wa Engelbert Kiondo wa mkoa wa kipolisi Temeke, amesema leo kuwa Vicent alikuwa akiishi Nzasa na amejinyonga kwa manila akiwa ndani ya stoo ya nyumba yao juzi saa 10:00 jioni baada ya kuambulia daraja la nne (Div IV), kinyume kabisa na matarajio yake.

Source: http://www.wavuti.com
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in Local News | No comments
Newer Post Older Post Home
View mobile version

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • Christiano Ronaldo and His 29 girlfriends List.
    Chr is tiano Ronaldo is famous as a great and cool football player. He play for England Manchester United Club, at age of 26 and he already...
  • Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.
    Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.                 Makumbusho ya  ka...
  • Tumehuzunika kidogo, Cesc Fabregas
  • Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA
    Computer System Analyst Grade I (Business Analysis) – One Post - (Re-advertised) E-Government Agency (EGA) Date Listed: J...
  • Post: Part-time journalist
    Post: Part-time journalist Job Description Timely and accurately collecting African real-time news and then integrate the manuscript ...
  • Tempetation
    An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage.    Jur...
  • University of Dar es Salaam among top 100 Universities in Africa
    The university of Dar-es-Salaam has ranked fourth among top 100 popular universities and higher learning institutions in Africa. This is acc...
  • Admission of Diploma holders into Higher
    TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES Admission of Diploma holders into Higher Education Institutions for the academic year 2013/2014. The T...
  • Community Relations Manager – (One Post)
    Community Relations Manager – (One Post) African Barrick Gold (ABG) Date Listed: May 15, 2013 Email Address: ...
  • Kim Kardashian awateka tena mashabiki kwa mavazi
    Kim Kardashian aliweza tena kuuteka umati waliohudhuria katika sherehe za kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko wa kuchangisha fedha kwa ajil...

Categories

  • Africa (1)
  • Announcement (13)
  • Biashara (17)
  • Breaking News (4)
  • Burudani (11)
  • East Africa News (19)
  • Education (12)
  • Entertainment (8)
  • Fashions (1)
  • Habari (41)
  • Health (1)
  • International News (14)
  • Jamii (11)
  • Jobs (120)
  • Latest Sports News (3)
  • Local News (59)
  • Makala (8)
  • Michezo (25)
  • Music (5)
  • News (12)
  • Scholarships (4)
  • Scholarships- Jobs (7)
  • Siasa (1)
  • Sport (64)
  • sports (18)
  • Technology (2)
  • Tetesi za Usajili (9)
  • usajili (1)

Blog Archive

  • ▼  2013 (335)
    • ►  September (9)
    • ►  August (18)
    • ►  July (23)
    • ►  June (27)
    • ►  May (91)
    • ►  April (53)
    • ►  March (41)
    • ▼  February (59)
      • Fergie: Let me move upstairs
      • NBC APPOINTS NEW MANAGING DIRECTOR
      • Tanzania Portland Cement launches new expansion fo...
      • Kenya boy, 13, gains fame for protecting livestock...
      • Do not fight over land, says National Lands Commis...
      • Monetary Boards in collaboration to support develo...
      • Rais Kikwete akagua Ukumbi wa Kisasa wa Mikutano w...
      • ‘Kitanda kimoja wanalazwa watoto 4, mliyoikuta leo...
      • Heart suggery in Tanzania coming Soon...
      • Je huu ndio mwisho wa Ufalme wa Barcelona???
      • Accounts Receivables Manager
      • 2. Chief Operational Officer
      • Youth Civic Engagement Assistant Project Coordinat...
      • Customer Services / Marketing Administrator ? Clot...
      • Kesi dhidi ya Sh. Ponda: Serikali yafunga ushahidi.
      • Gareth Bale Goals 2012/2013
      • Are Spurs a one-man team?
      • Mancini zaidi ya Benitez, Swansea yafanya mauji ko...
      • Beckaham zaidi ya Joe Barton Ufaransa
      • Rafael amazing goal vs QPR 2013 & Man united vs Qpr
      • Ajali mbaya ya mashindano ya Magari yajeruhi watu 33
      • Mil 142/= zapatikana Mama Salma akiongoza hafla ku...
      • Yanga Yaididimiza Azam, Manchester yaendelea kupaa!!!
      • Accountant for Charity
      • Volunteer Accountant for Charity
      • Vibwanga vya Masta wa majuu katika picha
      • Africa Specialist Tailormade Travel Consultant - C...
      • Barcelona Chaliiiii mbele ya Ac Milan
      • The growth rate of world manufacturing output rema...
      • A major progress has been made on the fight agains...
      • Vibwanga vya Mastaa wa Majuu
      • Wanafunzi wajiua kwa kufeli mtihani wa Kidato cha ...
      • SASA MKAZO NI KUMALIZA NAFASI YA 4 BPL!!
      • SASA MKAZO NI KUMALIZA NAFASI YA 4 BPL!!
      • Supermario Balotelli
      • Taarifa ya Katibu wa Bunge.
      • Post: Part-time journalist
      • Oscar Pistorius arrested over fatal shooting
      • Huyu ndiye Mrembo aliyeuawa na Bingwa wa Olympic y...
      • Museveni abuses uniform -Besigye
      • 2 *PhD* Positions in Programming Language-based Se...
      • Job Advert--BBC Worldwide Limited.
      • Analyst/Economist Vacancy
      • Tahadhari kuhusu kupandishwa vyeo kupitia ujumbe w...
      • Digitali yavunja ndoa za watu uswahilini
      • Pope Benedict will Resigns on February 28th, 2013
      • Michezo mbalimbali ya mwishoni mwa wiki! katika Pi...
      • Nigeria Mabingwa wapya wa Africa 2013
      • Baada ya Jamie Caragger kutundika Daluga...wajue w...
      • Master in Leading Innovation and Change from York ...
      • Vibwanga vya mastaaa wa majuu
      • Mwanafunzi wa miaka 9 mbaroni kwa kumwibia mwallim...
      • Drogba 's reaction after papis cisses goal
      • Heavy Equipment Engineers
      • Tanzania 1 Cameroon 0
      • FNB Celebrated one Year in Tanzania
      • TPA and Mombasa Porty Authorithy on mission to cur...
      • Mario Balotelli anza kungaa Italia
      • Maandalizi ya Super Bowl Sunday Yapamba moto
    • ►  January (14)
  • ►  2012 (162)
    • ►  December (42)
    • ►  November (70)
    • ►  October (50)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile